Athari za Madin ya Flouride Kwa Afya yako!!

Shirika la afya duniani(WHO) lilipendekeza kiwango cha fluoride kwenye maji ya kunywa kiwe 0.5-1 milligram/lita.

Kutokana na madhara makubwa yanayotokana na Fluoride, mataifa yaliyoendelea yanafanya mpango wa kuiondoa kabisa katika maji ya kunywa ( soma Dr Dean Burk, mgunduzi wa Biotin, amefanya kaz National Institute of Cancer marekani kwa miaka zaidi ya thelathini)

Fluoride iliyo katika dawa za meno imewekwa katika kiwango kikubwa sana ndiyo maana wameandika ukimeza bahati mbaya muone daktari. Pia watoto wasimamiwe wakiwa wanaswaki!

UCHAMBUZI WA MADHARA YA FLUORIDE

1.UBONGO

Uchunguzi wa kina wa kisayansi unaonesha kuwa kiwango kikubwa cha fluoride kinapunguza IQ( intelligence quotiet) kwa watoto ambao bado ubongo wao haujakomaa.

2. MIFUPA

Kiwango kikubwa cha fluoride kinadhoofisha mifupa na kupelekea watu wengi kuvunjika kirahisi haswa kwenye hips na kiwiko.


3. FIGO

Wenye matatizo ya figo wanashauriwa kutotumia fluoride kabisa. Ina madhara kwa figo zetu(fluoride induced nephrotoxicity)

4. MENO

Kiwango kikubwa cha fluoride hudhoofisha meno kwa kuyafanya yasiwe magumu hivyo kushambuliwa na bacteria kirahisi. Pia husababisha fizi kutoa damu. (Dental fluorosis)

5. THYROID

Fluoride husababisha watu kushindwa kutengeneza thyroxine hormone kwani huzuia Iodine isijishike kwenye kemikali inayotumika kutengeneza thyroxine hormone. Mwshowe tunaishia kupata goitre na matatizo mengine yatokanayo na upungu wa homoni hii mwilini

6. CANCER

Fluoride ni chanzo kikubwa sana cha kansa kwa binadamu. Inapojikusanya kwa muda mrefu matokeo yake ni mabaya sana. (Dr Dean Burk, USA)

Comments

  1. Asante Sana .but kuna dawa nzuri ya meno *aloevera toothgel*(bright) kama unahitaji napatikana 0627729510

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

Tanzanian entrepreneur develops innovative water filter